About

Moto ni jukwaa huru la waandishi kukutana, kubadilishana uzoefu, ujuzi, na kusaidia kukuza na kuendeleza jumuiya ya wanafasihi. Mkusanyiko huu utakaokuwa ukifanyika jumatano ya mwisho wa kila mwezi unawalenga waandishi wanaochipukia na wazoefu kama mahali pa kukutana na kujadili na kubadilishana mawazo kuhusu sanaa, taaluma na ufundi wao, vilevile kupata fursa ya kufanya kazi kwa pamoja ili kuendeleza jumuiya na taaluma ya uandishi kwa ujumla. Jukwaa hili ni huru kwa wote wa uzoefu, mitindo au tanzu za aina zote. Vilevile waandishi waliokwishachapishwa na wale ambao bado wanakaribishwa bila kujali kama ni waandishi wa kazi za utunzi na zisizo za utunzi, washairi, wanablogu, waandishi sinema, muziki n.k.

Moto is a forum for writers in Tanzania to connect with one another, share experiences, expertise, and help foster and be supported by the local literary community . A monthly discussion forum is held on the last Wednesday of every month.  This gathering aims to bring together budding and seasoned authors and provide a space to meet, discuss their craft, and work together to develop a community. The forum is open to all writers, regardless of experience and both published and unpublished writers are welcome. Writers of any style or genre are welcome including fiction, non fiction, songwriters, bloggers, screenwriters, poets etc.

Vilevile tutakuwa na nafasi kwa mwanajumuiya yeyote atakayetaka kusoma vifungu kutoka kwenye kazi yake, ili kupata mrejesho kutoka kwa wengine.

The forum will be an open space for discussions. There will also be the opportunity for any writer to read extracts of their work and if they wish, receive constructive critiques from the group.

Moto ni jaribio au mwanzo wa harakati za kujenga jumuiya ya wanafasihi yenye lengo la kusaidiana wenyewe kwa wenyewe na wakati huohuo kuendeleza jamii ya wanafasihi.

Moto will try to build a community to address the lack of support for writers and foster a literary community.

Leave a comment